Ukosefu wake walemaza utoaji wa chanjo ya COVID-19 barani Afrika

Get monthly
e-newsletter

Ukosefu wake walemaza utoaji wa chanjo ya COVID-19 barani Afrika

Chanjo milioni 38 pekee ndizo zimepokelewa katika bara la watu wapatao bilioni 1.2
Kingsley Ighobor
Afrika Upya: 
10 June 2021
Ukosefu wake walemaza utoaji wa chanjo ya COVID-19 barani Afrika
WHO
Limited supplies slow COVID-19 vaccination in Africa.

Ukosefu wa chanjo na utoaji chanjo isiyosawaizishwa unatatiza juhudi za kuchanja watu barani. Kufikia katikati ya Mei, ni chanjo milioni 38 pekee zilizopokelewa na nchi za Afrika. Katika idadi hiyo, chanjo milioni 23 zilikuwa tayari zimetolewa. 

Kufikia katikati ya Mei, ni chanjo milioni 38 pekee zilizopokelewa na nchi za Afrika. Katika idadi hiyo, chanjo milioni 23 zilikuwa tayari zimetolewa. 

Hata hivyo, takribani asilimia 83 ya dozi zilizotolewa hadi sasa ziko katika nchi 10 - Moroko, Nijeria, Uhabeshi, Misri, Kenya, Ghana, Zimbabwe, Angola, Tunisia na Senegali.

Moroko peke yake imetoa zaidi ya dozi milioni 10 kati ya milioni 23 zilizotolewa, ingawa Ushelisheli ina kiwango cha juu zaidi kwa kila mtu katika bara kwa kuwa imepata chanjo kamili ya asilimia 51 ya watu, kulingana na Shirika la Afya Duniani, Ofisi ya Kanda ya Afrika (WHO Africa).

Kwa kuzingatia idadi inayokadiriwa ya Afrika ya bilioni 1.2, dozi milioni 38 ni chache sana, wataalam wanasema. 

Pia, ulimwenguni, dozi bilioni 1.2 zimetolewa kufikia katikati ya Mei, na kufanya dozi milioni 23 za Afrika kuwa chini ya asilimia 2 ya jumla ya ulimwengu. 

"Afrika tayari inajaribu kuziba pengo la chanjo ya COVID-19, na pengo linazidi kuongezeka," alionya Dkt. Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO wa Kanda la Afrika, katika mkutano na waandishi wa habari mwezi Aprili.

Aliongezea: "Ingawa hatua zinapigwa, nchi nyingi za Afrika hazijasonga mbele zaidi ya mstari wa kuanzia. Upungufu wa bidhaa hii na vikwazo vya usambazaji vinafanya watu wengi katika eneo hili wasifikie chanjo za COVID-19. 

Dr Matshidiso Moeti, WHO Regional Director for Africa
Afrika tayari inajaribu kupata chanjo za COVID19 na hilo pengo lazidi kuongezeka
Daktari. Matshidiso Moeti
Mkurugenzi wa WHO Afrika

Habari njema

Habari njema ni kwamba utoaji chanjo unaendelea katika nchi 49 kati ya nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika. Na nchi 34 zimeripoti kuhusu kupungua kwa visa katika wiki iliyokamilika tarehe 9, Mei. 

Kwa ujumla, ingawa maambukizi yaliongezeka kwa 33,794 katika wiki ya 3-9 Mei, takwimu hizi ziliwakilisha "kupungua kwa asilimia 14.5 ikilinganishwa na wiki iliyotangulia," WHO Africa walisema.

Habari nyingine njema ni kwamba takwimu za WHO zinaonyesha kuwa maambukizi barani Afrika ndiyo yako chini kuliko eneo lingine lolote. Kati ya visa milioni 160 vilivyothibitishwa vya COVID-19 ulimwenguni, visa milioni 3.3 (asilimia 2.9) viliripotiwa barani Afrika.

Ingawa hivyo, wataalam wa magonjwa wanashawishi kuwa kuchanja idadi kubwa ya watu, bila

kujali msambao wa sasa, kunahitajika ili kukomesha janga hili.

Kulingana na WHO Africa, kuna ongezeko la kiwango cha maambukizi katika angalau nchi 11 za Afrika, ikijumuisha Angola, Komoro, Eritrea, Eswatini, Lesotho, Mauritania, Nijeri, Afrika Kusini, Uganda na Zambia.

"Afrika Kusini imeanza kuwa na ongezeko la visa vya kila wiki baada ya zaidi ya miezi miwili ya kupungua," ilisema ripoti ya WHO Africa

Nchi 10 ambazo zimepata chanjo ya watu wao zaidi zimetumia angalau asilimia 65 ya bidhaa hii, ikimaanisha kuwa zisipopata tena bidhaa hii kwa haraka, zitakuwa zimebakisha chanjo chache za kuendeleza shughuli zao za chanjo.

Ongezeko kubwa la chanjo nchini Afrika Kusini litaathiri idadi ya jumla ya Afrika, ikizingatiwa kuwa nchi hii inachangia kwa karibu asilimia 35 ya jumla ya visa barani.

Jitihada za chanjo ya serikali ya Afrika Kusini zilitatizwa na aina mpya ya virusi vya korona, ambayo chanjo ya AstraZeneca haikuweza kukabili vizuri.

ulimwenguni, dozi bilioni 1.2 zimetolewa kufikia katikati ya Mei, na kufanya dozi milioni 23 za Afrika kuwa chini ya asilimia 2 ya jumla ya ulimwengu.

Kwa sababu hiyo, serikali ya Afrika Kusini ilisitisha matumizi ya AstraZeneca na kuagiza chanjo ya Johnson & Johnson ambayo imeonekana kuwa nzuri dhidi ya aina mpya ya virusi hivi. 

Hata hivyo kufikia Aprili, miezi miwili baada ya kuanza kutoa chanjo ya J & J, habari zilichipuka kuwa watu wachache waliotumia chanjo hiyo huko Marekani walikuwa wameganda damu, na kulazimisha serikali ya Afrika Kusini kusitisha matumizi yake. 

Chanjo inaweza kuongezeka katika miezi ijayo katika nchi ya Afrika Kusini; inatarajia kupata zaidi ya dozi milioni 1 za chanjo ya Pfizer mwishoni mwa Mei. Nchi hii imeanza tena matumizi ya J & J, kufuatia kuidhinishwa kwake mwezi Mei na Utawala wa Chakula na Dawa wa Marekani.

Kwa sasa, kusita kupata chanjo na Waafrika kulikozungumziwa sana hakutatokea, kulingana na utafiti uliofanywa na Africa CDC na London School of Hygiene & Tropical Medicine mwezi Desemba iliyopita kutambua "mianya ya kimaarifa, imani za kitamaduni, na mitazamo ya kufahamisha hatua za kutolewa kwa chanjo barani kote. ”

Utafiti huo ulionyesha kuwa hadi asilimia 79 ya wahojiwa walikuwa tayari kupokea chanjo ya COVID-19 bora imeonekana kuwa salama na yenye ufanisi. 

Kikwazo ni kuwa matayarisho ya kupokea chanjo yanatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine. Kwa mfano, huku asilimia 94 ya WaHabeshi na asilimia 93 ya WaNijeria wangepokea chanjo kwa hiari, ni asilimia 65 pekee ya WaSenegali na asilimia 59 ya WaKongo walisema wangezipokea.

Africa CDC ilisema kuwa "kabla ya janga la COVID-19, kulikuwa na kupungua kwa kiwango cha kukubalika na kupokelewa kwa chanjo kwa sababu ya kushukiwa kuhusu ufanisi na usalama na kuenea kwa habari potofu kuhusu chanjo.