Matokeo ya COP27: Tathmini kuhusu hatua zilizofikiwa, fursa zilizopitwa

Get monthly
e-newsletter

Matokeo ya COP27: Tathmini kuhusu hatua zilizofikiwa, fursa zilizopitwa

Hazina ya kusaidia hasara na uharibifu imekaribishwa, haja ya kushughulikia ukabilifu na utekelezaji wa hazina ya kusaidia walio katika hatari zaidi
Afrika Upya: 
15 December 2022
Fazal Issa
If you can't read now, just listen to the audio version: 
Fazal Issa Climate and Environment Programme Manager at the Embassy of Ireland, Tanzania
Fazal Issa

COP27 iliyohitimishwa hivi majuzi, na ambayo ilifanyika jijini Sharm el-Sheikh, Misri, ilileta pamoja zaidi ya watu 35,000 kutoka kote ulimwenguni kujadili hatua muhimu za kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa.

COP27, iliyopewa mada ya “COP ya Afrika” na “COP ya Utekelezaji,” iliibua matarajio kwamba maamuzi ya makongamano yaliyopita, yanayoakisi mahitaji na vipaumbele vya nchi zilizo hatarini zaidi, yataanza kutekelezwa.

Baada ya wiki mbili za mazungumzo, COP27 ilipitisha Mpango wa Utekelezaji wa Sharm el-Sheikh "SHIP" kama uamuzi mkuu wa kuongoza hatua kabambe za mabadiliko ya hali ya hewa.

Wengi wanaona mpango huo kama njia ya kuendeleza juhudi kutoka kwa makongamano ya awali, kama vile hazina ya hasara na uharibifu. Hata hivyo, wengine wanahisi kuwa mpango huo umepungukiwa kwenye hatua za uzuiaji.

Jambo kuu kwenye COP27 lilikuwa uamuzi wa kihistoria wa kuanzisha hazina kwa ajili ya kukabiliana na hasara na uharibifu. Ni hatua muhimu kwa sababu inakuja baada ya takriban miongo mitatu ya kuomba na inaweka mfano kwenye haki kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

The highlight of COP27 was the Jambo kuu kwenye COP27 lilikuwa uamuzi wa kihistoria wa kuanzisha hazina kwa ajili ya kukabiliana na hasara na uharibifu. decision to establish a fund for responding to loss and damage.

Hata hivyo, muundo na utekelezaji wa hazina ya kusaidia walio hatarini zaidi, hasa katika Nchi Zinazoendelea na Mataifa ya Visiwa Vidogo, bado haujashughulikiwa.

Kongamano hilo halikufikia mafanikio mengi kuhusu uzuiaji. Halikuweza kufikia makubaliano, kwa mfano, juu ya kukomesha mafuta ya makaa ya visukuku vingine au kuweka makataa ya utoaji wa hewa chafu.

Hii inazuia juhudi za kupunguza wastani wa ongezeko la joto duniani hadi 1.5°c (juu ya viwango vya kabla ya viwanda). Ili kufikia lengo hili, tunahitaji upunguzaji wa haraka, wa kina na endelevu wa uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 45 (ikilinganishwa na viwango vya 2010) ifikapo 2030.

Kama ambavyo imekuwa kwa miaka mingi, washiriki walionyesha wasiwasi kuhusu utoaji wa fedha zinazoahidiwa za hali ya hewa, hasa kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. COP15 ilitoa robo tu ya dola bilioni 100 kwa mwaka zilizoahidiwa kwa nchi zinazoendelea ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mamlaka zinatarajia kuendeleza mchakato wa kuanzisha lengo jipya la ufadhili wa mabadiliko ya hali ya hewa na lengo la kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa mwaka ujao. Hii inapaswa kuongozwa na ripoti za kisayansi na kuonyesha mahitaji halisi ya nchi zilizo hatarini zaidi.

Kwa mara ya kwanza katika historia yake ya miaka 27, kongamano hilo lilitenga siku moja kwa mada ya kilimo.

Kwa hivyo, lazima tuchukue hatua za haraka na kwa ujasiri kuokoa uwepo wa ubinadamu sasa na kwa vizazi vijavyo.

Matokeo muhimu yalikuwa ni kuzinduliwa kwa mkakati wa Chakula na Kilimo kwa ajili ya Mageuzi Endelevu. Mkakati huo unalenga kuboresha wingi na ubora wa michango ya fedha za mabadiliko ya hali ya hewa ili kubadilisha mifumo ya kilimo na chakula ifikapo 2030.

Jukumu la wahusika wasio wa serikali lilitambuliwa tena - hasa vijana, jamii za mitaa, watu wa kiasili, miji na asasi za kiraia. Wote wamekuwa wakitekeleza majukumu muhimu katika kuzitaka serikali kutekeleza ahadi zao.

Kama isemwavyo, "mwisho wa COP moja ni mwanzo wa maandalizi ya ijayo." Nchi na watendaji wasio wa serikali, kwa hivyo, watahitaji kujipanga upya, kutathmini matokeo muhimu kutoka kwa COP27 na kubainisha vipaumbele vya COP28.

Vipaumbele vyao kwa hakika lazima vijumuishe kubuni na kutekeleza hazina ya hasara na uharibifu, kukamilisha uanzishwaji wa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya hali hewa na kuendeleza mchakato mpya wa kutathmini lengo la hazina ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Muhimu vilevile, watatarajia utoaji wa ahadi za ufadhili wa mabadiliko ya hali ya hewa na malengo yaliyoimarishwa ya kupunguza uzalishaji hewa chafu kupitia Michango iliyodhamiriwa ya Kitaifa na juhudi zingine za muungano wa nchi mbili na kimataifa.

Huku tathmini ya kwanza ya kimataifa ikitarajiwa kufanyika katika COP ijayo, itakuwa muhimu kwa nchi kutathmini na hatimaye kuimarisha hatua na usaidizi wao kulingana na majukumu yao chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya hali ya Hewa (UNFCCC).

Kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anavyosema, "Sayari yetu bado iko kwenye chumba cha dharura na ubinadamu uko kwenye barabara kuu ya kuzimu."

Kwa hivyo, lazima tuchukue hatua za haraka na kwa ujasiri kuokoa uwepo wa ubinadamu sasa na kwa vizazi vijavyo.

More from this author